MAONESHO YA KILIMO NA MIFUGO (NANENANE), VIWANJA VYA TASO-THEMI HILL NJIRO ARUSHA-2013


Hiya ni baadhi tu ya mabanda ya halmashauri mbalimbali zilizokuwepo viwanjani 





Utaalamu wa namna ya utunzaji na ustawishaji bora wa bustani za mbogamboga





Umati wa watu na pilikapilika za kila mmoja za kuzunguka huku na huko...





Hata wenye watoto wadogo waliamua wawabebe tu na kujanao ndani ya viwanja hivi....





Hata wageni wa kila aina kutoka nje ya nchi nao pia walikuwepo kwa wingi ndani ya viwanja hivi.





Huu siyo mzigo wa kuni wala wa mihogo! Na wala hizi siyo kuni. Biashara ya mtu hii, Wakwetu. Ni mizizi ya mmea ambayo kwa wakazi wengi wa Arusha wanaifahamu kwa jina la mkongoraa. Ni dawa inayotafunwa tu kama mizizi ya mihogo au viazi. Eti inadaiwa kazi yake kubwa ni kusafisha figo; na pia kwa wanaume 'inawaongezea' changamoto za unyumba. Mh! Haya ndugu maasai naona unarejeshewa chenji baada ya kujinunulia mkongoraa....  





Vihoja na vimbwanga vya wanasarakasi navyo havikukosekana. Gurudumu la baiskeli linazungushwa kwa kasi juu ya mgongo wa binadamu...





Ufugaji bora wa wanyama wa aina mbalimbali nao pia ulikuwepo. Hawa ni ng'ombe wa maziwa





Hata Sungura nao walikuwepo....


No comments: