HAKUNA UBAYA WOWOTE KUKUMBUSHANA KWA MARA NYINGINE, HATA KAMA WIKI KADHAA ZILIZOPITA NILIBAHATIKA KUKUDOKEZA JUU YA HILI....


Wakwetu, hali ya hewa ya Mji wa Arusha pamoja na majirani zake (mikoa ya Kilimanjaro na Manyara) kwa sasa bado ni ya baridi sana, kiasi ambacho panahitajika wakati wote kujitahidi kuilinda na kuihifadhi mno miili yetu dhidi ya hali hii. Mzahamzaha, siku zote mwisho wake ni kule kwenye ule usemi wa "majuto ni mjukuu!" Kinga na tahadhari ni bora mno, kuliko mateso ya nimonia, kifua cha baridi na hata asma. Baridi hii wala haituhitaji kamwe kuitafutia misifa mbele ya wanadamu wenzetu, kwa kujionesha kwamba wala hatuiogopi! Na tena kwa wale wenye watoto wadogo, huu ndio wakati hasa wa kuwa makini na wakali kwelikweli ili kuhakikisha muda wote miili ya watoto wetu kuanzia juu kichwani hadi chini miguuni imehifadhiwa vema kwa mavazi ya kuwalinda dhidi ya ubaridi huu . Vinginevyo, yakimkuta ya kumkuta mwanao basi uelewe wazi kwamba itakubidi uzisimamishe kwa muda shughuli zako zote ili kumhangaikia huku na kule mahospitalini hadi pale atakapopata nafuu au kupona kabisa...



Shuka nzito mfano wa hili, au blanketi, ni muhimu mno wakati wa usiku kitandani...






 

Masweta na makoti mfano wa haya nayo pia ni muhimu sana mwilini muda wote, usiku na mchana






Soksi nzito za miguuni...





Kofia nzito a.k.a bosholi

Wala usimwonee aibu wala haya mtu yeyote yule. Katika kipindi hiki soksi nzito za mikononi nazo pia ni muhimu mno... Wakwetu, jipigilie tu mikononi; na hasa kwa wale waamkao asubuhi sana na kurejea nyumbani jioni au usiku ambapo kibaridi ndipo huwa kimezishika vema hatamu zote za mwili.

Mpini Wa Shoka umetoa ushauri tu, lakini utekelezaji wote ni juu yako mwenyewe...

No comments: