JENGO JIPYA LA MSIKITI WA MABANIANI (tample)-ARUSHA

 

Limejengwa pembezoni tu mwa mahali lilipo jengo lao la zamani. Ni maeneo ya Jirani na uwanja wa michezo wa shule maarufu ya Sekondari ya Arusha (Arusha Sec). Na pia ni eneo lililo jiranijirani tu na ofisi za NSSF-National Social Security Fund na jumba maarufu la Senema jijini Arusha la Metropole 


Jengo hili jipya pamoja na kuwa na sehemu ya ibada (upande huu wa mbele unaoonekana), lakini pia lina sehemu ya hosteli kwa wageni (kwa upande wa nyuma mwa jengo). Na pia kwa mbele pametengenezwa eneo kubwa na zuri la kuegeshea maghari kama unavyopaona   





Kwenye ukuta panapoonekana watu wakitembea, ni uzio wa eneo la jengo (tample) la zamani ambalo pia ndani yake kuna upande wenye hospitali maarufu mjini Arusha ya Shree Hindu. Majengo haya mawili yanatenganishwa na barabara ya magari (wanakopita watu), ambayo inatokea eneo la Metropole-Barabara ya Sokoine (zamani Uhuru road) na kuteremka hadi mtaa wa Jamhuri (Jaluo street)-Kata ya Daraja mbili, Faya na hata hadi Sinoni, N.M.C Ungalimited na Sokon One




Pembezoni mwa jengo jipya kuna mto wa maji ambapo kwa miaka mingi wananchi wa mitaa na vitongoji vya maeneo ya Kata ya Daraja mbili, Faya na hata Sinoni na Ungalimited wamekuwa wakiyatumia maji yake kwa ajili ya kustawishia bustani zao za mbogamboga na hasa mchicha (kama zinavyoonekana kwa uchache). Kidaraja hiki kidogo kiliwekwa na ndugu hawa wa kibaniani kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi watembeao kwa miguu kuvuka bila ya utata. Lakini matokeo yake, baadhi ya wenye magari na hasa teksi wakaanza kulitumia daraja hili kwa kukatisha na magari yao kuelekea pande za Shule ya Sekondari ya Arusha Day na Themi (huko anakotokea huyo mama anayevuka daraja) kwa sababu ni njia ya mkato sana. Ndipo ndugu wa kibaniani wenye kumiliki ma-tample haya mawili (la zamani na jipya) wakaamua kuweka vyuma juu ya daraja ili kulipunguza ukubwa uliyowashawishi wenye magari kupita hapa, kiasi cha kufikia hata wakati fulani kutaka kuliangushia mtoni daraja hili    


No comments: