ELIMU NI MUHIMU... ELIMU NI MWONGOZO...

Wakati bado nina rundo la mavituz kibao ya ndani ya Jiji la Dar es salaam, ambayo bado sijayamaliza kukutupia; hebu turudi kidogo ndani ya Jiji la Arusha. Hapa ni katika Chuo cha Mafunzo ya Uandishi wa Habari pamoja na Utangazaji wa Redio na Televisheni, kwa ufupi A.J.T.C, kilichopo maeneo ya Fidi Fosi (Field Force Unity-FFU)-jirani na eneo la KwaMromboo-Arusha. Ni miongoni mwa Vyuo ambavyo kwa miaka kadhaa sasa kimekuwa kikitoa wanataaluma wengi katika tasnia ya habari na utangazaji. Hata Mpini Wa Shoka nao umefanikiwa kupiga buku katika chuo hiki, na bado unaendelea kupiga zaidi na zaidi kwa kadiri ya nafasi inavyouruhusu. Lakini kwa siku za hivi karibuni Chuo hiki cha A.J.T.C kiliingia katika matata, baada ya kuenezwa kwa uvumi mkubwa kwamba hakikusajiliwa, kiasi cha kuwafanya hata baadhi ya wahitimu wa kipindi cha nyuma na wale waliokuwa wakiendelea na mafunzo yao kuinua simu na kuulizia wizarani kunakohusika na elimu. Hata hivyo, uvumi huo hauna ukweli wowote kwani chuo hicho kimesajiliwa na kinatambulika na wizara kwa muda mrefu tu. Tatizo lililokuwepo ni kwamba vyeti vya wahitimu ndivyo ambavyo havikuwa vikichapwa pamoja na namba ya usajili wa Chuo. Kwa sasa, wahitimu wote wanatakiwa kufika chuoni na vyeti vyao ili vifanyiwe marekebisho katika kasoro hiyo ndogo....  

Huyu ndiye Mkuu wa Chuo hiki Bwana Joseph K. Mayagilla. Usiutazame ujana wake ukakuzubaisha, kichwani vitu vya maana vimelala hapa. Hata mimi amenipiga shule ile mbaya. 

 


Sehemu ya wanafunzi wakiwa katika mojawapo ya madarasa ya chuo hiki cha AJTC-Arusha Journalism Training College wakipiga buku na kujadiliana hapa na pale. Huenda mashuhuri wa baadaye katika vyombo mbalimbali vya habari wamo humu! Nani anayejua!





Anaitwa Andrew Ngobole. Ni mmojawapo wa walimu. Hapa Chuoni ni mwalimu mlezi wa wanafunzi. Lakini kwangu, ni mwalimu zaidi wa sheria na maadili yanayotawala uwanja wa tasnia ya habari na utangazaji. Naye pia alinipiga darasa wakati wa hekaheka za kuisaka diploma kwa miaka miwili. Naye pia ni kijana tu, lakini kazi inafanyika kwa viwango.

 

 

 

Ujumbe wangu, "Hata kama tayari uko ndani ya chombo cha habari na unafanya kazi, na tena una jina kubwa linaloheshimika sana, lakini Wakwetu, ni vema kupita kwenye chuo kama hiki ili uweze kujiamini na kufanya kwa ubora zaidi. Umaarufu mkavumkavu tu peke yake hautoshi. Kuna siku unaweza ukalikoroga, ukajikuta linakushinda kulinywa!" 

No comments: