ZUNGUKA KIDOGO MJINI NA MPINI WA SHOKA.
Hapa ni maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam, Mpini Wa Shoka ukiwa ndani ya Daladala ukitokea pande za Magomeni ukielekea katikati ya Jiji. Maghorofa yanayoonekana vema mbele yako, yote yapo eneo la Kariakoo. Jengo la rangi ya Njano na Kijani ni la klabu maarufu na kongwe nchini Tanzania- Young Africans (Yanga), ambapo hapa pia ndipo ulipo uwanja wao wa mazoezi (mbele kidogo ya vijengo vidogovidogo vya rangi ya Kijani na Njano). Sasa nyasi hizi ndefu zinazoonekana hapa jirani yako kabisa, ndipo ulipo uwanda wa bonde la mto Msimbazi; kwa hivyo, sehemu kubwa ya nyumba zote zinazoonekana jirani na nyasi hizi zimejengwa ndani ya uwanda wa bonde la mto huu! Ndiyo maana mafuriko ya bonde hili yakitokea, basi nyumba zote hizi huwa ndani ya matata makubwa. Maji hujaa kila mara ndani ya nyumba hizi, lakini eti wenyeji wanajidai wamezoea! Hata wakiondolewa na serikali, baada ya siku kadhaa wanarejea kinyemela! Na baadhi ya wapiga porojo wa kisiasa husimama na kuwaunga mkono kwa kigezo za haki za binadamu. Lakini maafa yakitokea, lawama zote ni kwa serikali "ooh! Haiwajali wananchi wake!"
Hata Dar napo kuna sehemu inakofahamika kwamba ndiko Mjini. Hapa sasa ndipo mjini ndani ya Jiji la Dar es salaam. Siyo maeneo ya Kariakoo ulikozoea kufikiria kila siku...
Haya ni baadhi ya maeneo hayo ya katikati ya jiji (mjini)...
Hapa ni Samora Evenue (maeneo ya mtaa wa Samora) kwenye picha la sanamu la askari, jirani kabisa na posta mpya. Maeneo haya na ya jirani na hapa, ndipo yanakopatikana karibu majengo na ofisi za wizara zote za nchi ya Tanzania, na pia Ikulu kwa Mr President na Bandari kuu pamoja na hoteli kadhaa maarufu.
No comments:
Post a Comment