MABASI YAENDAYO KASI-KAZI ZINAENDELEA KUPAMBA MOTO.

Katika maeneo kadhaa ambayo Mpini Wa Shoka ulifanikiwa kupitapita ndani ya Jiji la Dar es salaam, nilifanikiwa kuziona hekaheka chungu nzima. Lakini kubwa kabisa ni lile la kuendelea kuziboresha na kuzipanua zaidi barabara nyingi tu, ambazo kwa kiasi kikubwa zimeufanya msongamano wa magari (traffic jam) uliokuwa ukizidi kukera kila kukicha sasa upungue kwa kiwango fulani ndani ya jiji hili kubwa nchini Tanzania. Lakini pia harakati za ujenzi wa njia (barabara) mpya za huduma ya mabasi yaendayo kasi nazo zinazidi kupamba moto. Hapa ni mojawapo ya maeneo ambayo Mpini Wa Shoka ulifanikiwa kukunasia mbili tatu za kazi za ujenzi wa njia (barabara) hizo kwenye barabara kubwa ya Morogoro (Morogoro Road

Mafundi kazini na mitambo yao maeneo ya Magomeni.





Nondo zilizosimama kwenye zege iliyomiminwa vema ndipo zinakojengwa njia na vituo vya mabasi hayo yaendayo kasi. Lami inayoonekana pembeni ni ya barabara ya Morogoro (Morogoro Road)

 

 

Moja ya magari yaliyobeba mitambo yakiwa kazini wakati wa ujenzi 




Mawe makubwa ya zege yakiwa yamewekwa ili kuwadhibiti madereva wakorofi hasa wale wa daladala wanaopenda kuvamiavamia ovyo tu ndani ya maeneo ya ujenzi ambayo yapo katikati ya barabara, katika hekaheka za kukwepa msongamano (Jam). Hapa ni kwenye mataa ya kuongozea magari (Traffic lights) maeneo ya Kichangani kwenye makutano ya barabara za Morogoro (Morogoro Road) na Kawawa. Vinara vya msikiti mkubwa wa Kichangani vinaonekana vema kwenye picha ya juu na ya chini. 




No comments: