NDANI YA JIJI-DAR


Ndani ya stendi kuu ya mabasi (Ubungo Terminal) Dar es salaam. Miaka ya nyuma wakati eneo hili ambalo lilikuwa ni kituo cha mabasi ya usafiri ndani ya Jiji la Dar es Salaam (UDA), lilipokuwa likibuniwa ili kufanywa stendi kuu ya mabasi ya mikoani, porojo chungu nzima ziliamka huku na kule. Wengine oooh, ni nje sana ya Mji..! Wengine Oooh, hapafai kwa sababu ni shamba (porini)..! Na wengine na wengine na wengine nao wakaweka porojo zao za kila aina. Lakini tangu stendi ilipohamishwa rasmi kutoka eneo la Zanaki katikati ya Jiji na kuletwa hapa, sasa hivi wapiga porojo hao wamebaki midomo wazi! Hata stendi yenyewe sasa haitoshi tena kwa idadi kubwa ya mabasi yanayoingia na kutoka hapa Ubungo; na hata eneo lenyewe la Ubungo sasa pamekucha ile mbaya. Wakwetu, ukisikiliza sana porojo za wapiga porojo ambao siku zote kwao kila kitu ni hakifai tu mbele ya macho na masikio yao, mara zote utajikuta ukishindwa kutekeleza mipango ya maana kabisa. Ndiyo maana leo hata tunapata viongozi na wabunge ambao kauli na maneno yao ukiyafanyia utafiti wenye akili utagundua ni walewale tu mabingwa wa kupinga kila kitu hata kama ni kizuri na chenye manufaa kwa kiasi gani kwa jamii. Ukiambiwa neno, basi na wewe weka na la kwako kichwani! Siyo yeye akisema hapa ndani ya choo hiki kilichotapakaa mikojo eti panafaa na ni salama kabisa kwa kulala usiku kucha hadi asubuhi, na wewe kazi yako ni kumshangilia na kuitikia tu ndiyo, na kisha unajilaza juu ya mikojo! Tafakari na upime kwanza. 


Ubungo Terminal (stendi kuu) kwa nje mapema asubuhi.


 


Stendi ya mabasi-Temeke




Stendi ya mabasi-Mbagala Rangi tatu. Mvua ikinyesha hapa, huwa ni sokomoko na heka heka tupu ya madimbwi.

 



Mbagala Rangi tatu-Asubuhi kwenye vituo vya daladala; tunasubiri usafiri wa kwenda huku na huko kwenye harakati na kazi zetu mbalimbali... Hapa wengine tumepozi tu, wala hatueleweki (hatusomeki) kama nasi pia ni abiria ama vipi!

No comments: