KARIBU LINDI-TANZANIA

Mpini Wa Shoka ulifanikiwa kuokota mbili tatu za mkoa wa Lindi wakati wa safari yangu ya Dar-Mtwara-Dar....

Ni mkoa ambao nao pia uko katika mwambao wa bahari ya Hindi, kama ilivyo pia kwa mkoa wa Mtwara. Kwa hivyo, unapoanza kuingia katika mkoa huu utapokelewa na fukwe mwanana kama hizi.





Ndani ya stendi (kituo) kuu ya mabasi biashara na harakati mbalimbali nazo zinaendelea kama kawaida. Korosho kibao. Ni wewe tu na mfuko wako kama unakuruhusu.





Mitaa mbalimbali ya Mji wa Lindi na vichochoro vyake...

Nako pia mvua zinapiga ile kisawasawa...



Zana za kazi kama hizi, nazo pia zipo. Sasa sijui hapa ni duka la kuziuza..! Au hapa ni kiwanda cha kuzitengeneza..! Au ziko kwenye maegesho (parking)..!




Bado taswira ya majengo ya miaka mingi ya zamani kabisa kabla ya Uhuru wa Tanzania (Tanganyika), inaonekana wazi... Ingawa hata mapya ya kisasa yanayovutia, nayo pia yapo.





Kandokando mwa bahari...

Ni safu ya miti ya mikoko; miti yenye asili ya kuota pembezoni mwa maji ya bahari. Hapa ni eneo ambalo maji ya bahari yanaonekana yameondoka muda siyo mrefu sana. Kawaida ya maji ya bahari huwa yanaondoka kabisa katika eneo fulani, na kisha hurejea polepole baadaye sana na kujaa kabisa! Na mara nyingi huwa yanaondoka nyakati za mchana.





Kwa harakaharaka waweza kufikiri hiki ni kitu gani hasa? Ni bwawa la kufugia Samaki! Au ni bwawa la maji machafu katika Mji huu wa Lindi! Hapana. Hivi ni vitalu vilivyojaa maji ya bahari ambavyo hapa huvunwa chumvi ya kutumia majumbani, wakwetu. Mbona umetumbua mimacho! Ina maana hauniamini? Piga simu Kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi umuulize. 

 

 

 

Maelekezo kwenye mzani wa kupimia magari; Lindi.

Ukipotea ni juu yako.

 


No comments: