Huu ni msimu wa kujiandaa na usambazaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima.... Mpini Wa Shoka mwaka huu umebahatika kushiriki katika zoezi hilo katika mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na mawakala wa pembejeo...Kwa sasa mawakala wanachukua pembejeo kutoka katika vituo maalumu vya utayalishaji, na kuzipeleka katika maduka maalumu pamoja na ofisi za vijiji, kabla ya zoezi zima za ugawaji wa pembejeo hizo kwa wakulima halijaanza rasmi.......
Hiki ni mojawapo ya vituo vya utayarishaji wa mbegu bora za mazao kilichopo eneo la Ngaramtoni ya Juu, ambavyo mawakala walioidhinishwa hufika kwa ajili ya kujipatia mbegu na kuzipeleka kwa wakulima wa maeneo yao wanayoyahudumia..
Karibu sana dukani
Hapa ndipo eneo la utayarishaji wa mbegu
Mbegu zikiwa katika vipimo na vifungashio vyake.
Tayari zimekwishafungwa. Kila paketi moja ina uzito wa kilogram 2.
Ndani ya mifuko hii ndimo paketi za mbegu huwekwa tayari kwa kuchukuliwa na mawakala
Baadhi ya zana za kilimo kwa ajili ya kupandia, kuwekea mbolea na hata kupalilia na kuvunia zikiwa zimeegeshwa katika kituo hiki tayari kwa kazi
Haya ni matreka ya kituo hiki. Bila ya kilimo ni hatari....kilimo kwanza ili kujiepusha na hatari za njaa
No comments:
Post a Comment