TUMALIZANE NA YA OLD MOSHI...

Shule ya sekondari Moshi (Old Moshi Sec) ina jumla ya wanafunzi wapatao 826 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, ambapo wote ni wa kiume. Na kati ya hao, 303 ni wa kidato cha 6 ambao ndio waliohitimu...

 

Hii ni sehemu tu ya idadi ya watu waliohudhuria kutoka pande mbalimbali za Tanzania, wazazi, walezi, ndugu, jamaa na hata marafiki...

Na kama ningelikuwa sijaaga nyumbani kwamba nitakuwepo kwenye maafali haya, basi huenda ningeweza kuumbuka mchana kweupe, maana ningekamatwa tu na huyu shemeji yangu mwenye nguo ya njano ambaye tuligongana ghafla tu macho kwa macho! Lakini kwa bahati nzuri hata familia yangu nayo pia ilikuwepo hapa...

 

 

Hawa ni sehemu ya waalimu na wafanyakazi wa shule hii pamoja na wageni waalikwa kwenye meza kuu... 




Baadhi ya wahitimu wa kidato cha 6 wakiwa wamepouz...





Ndipo likaja igizo hili la kukata na wembe....

Ni stori ya kifo cha marehemu. Unataka kujua historia ya maisha ya marehemu? Hebu jaribu kupitisha macho kwa makini, huenda ukabahatisha ni kitu gani hasa kilichomuua.. 

Baada tu ya kumaliza kidato cha 6, maisha yake sasa yakawa ndio haya (aliyevaa fulana ya rangi ya njano yenye miraba myeusi)


Kugonganisha wakina dada kwake kilikuwa ni kitu ch kawaida tu...




Ulevi nao ulikuwa umemteka vilivyo. Hata swahiba (rafiki) wake mkubwa alipokuwa akijaribu kumsihi, ilikuwa ni patashika ya maneno mazito aliyomporomoshea....




Hata baba yake mzazi (aliyekaa) alimjibu ovyoovyo tu alivyopenda yeye kwa sababu alidai alikuwa na elimu kubwa zaidi kumshinda....Rafiki yake alipomsihi, alimwambia kama anamwona huyo mzee ni wa maana sana basi yeye ndiye ageuke awe mwanawe...!



Kisha jamaa anaimba kwa hisia akimuaga marehemu...




Huu ndiyo mwili wa marehemu (kigaragosi)




Kisha ikawa ni nafasi ya mgeni rasmi...

Bwana Emanuel Cosmas Kavishe kutoka Trust Bureu de Change ya mjini Moshi, ambaye pia aliwahi kusoma katika shule hii, akimwakilisha mgeni rasmi ambaye ni mkurugenzi wake. 



Hapa akimzawadia noti taslimu mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika matokeo ya kidato cha pili, Babuu.





Dogo, Babuu, akiwa na noti zake mkononi. Wazazi na wageni wengine nao pia walijitokeza kumjaza manoti zaidi Bwana mdogo...




Kisha ikapita burudani kidogo ya hawa jamaa wa kidato cha 4...

Wanajiita wachafu a.k.a wasafi. Kazi yao ni kucheza tu (madansa)... Ni Gabriel Erasto na Innocent Maiko.




Kisha mambo ya zawadi na vyeti yakafuata...

Mwalimu Mkuu msaidizi, Mwl Saro, akipewa zawadi na mgeni rasmi. Huyu mwalimu kila aliposimama tu, wahitimu wote wa kidato cha 6 walimshangilia kwa nguvu... 




Huyu ndiye mkali wa masomo kwa kidato cha 6. (Yasome mwenyewe kwenye boksi uyaone). Kijana kutoka Mwanza; anaitwa Jeremia Shigella.




Hawa ni wakali wa masomo kwa kidato cha 5 wakiwa wamezawadiwa... 




Na hawa ndiyo wakali wa masomo kwa kidato cha 6 wakiongozwa na mkali Jeremia Shigella katikati na boksi lake la zawadi..





Kiongozi Mkuu wa wanafunzi Charles Gidabit Gisinyaw na wanafamilia wake...





Ni raha tupu baada ya kukabidhiwa cheti cha kuhitimu kidato cha 6....

Mwanafunzi Saidi akiwa na furaha ya kutosha pamoja na mama yake mzazi... 


Hapa akivishwa taji na dada yake....

No comments: