MOJAWAPO YA MIRADI YA TASAF NDANI YA JAMII-WILAYANI ARUSHA...
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ilkiushin, Wilaya ya Arusha (Arusha Vijijini), Mh. William
Samwel Kalama, akifungua rasmi Semina iliyofanyika hivi karibuni katika Kijiji
chake, kwa kuwakaribisha wawezeshaji na wanasemina, wakati wa Semina juu ya mradi ulioibuliwa na wanakijiji
wenyewe wa Kijiji cha Ilkiushin, mradi wa utengenezaji wa barabara, ambao
unawezeshwa na TASAF.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ilkiushin, Bwana Denis
Mcharo, akiusikiliza kwa makini ukaribisho wa Mwenyekiti wa Kijiji chake, Mh. William
Samwel Kalama, kwa
wawezeshaji pamoja na wanasemina.
Humu ndimo Semina hii ilipofanyikia. Hili ni
jengo la ofisi za Kijiji cha Ilkiushin.
Toilet ya
Ofisi ya Kijiji….
Mmoja wa wawezeshaji wa Semina hii, kiongozi wa
upembuzi shirikishi katika kuwezesha jamii kuibua miradi watakayoitekeleza
wenyewe wakiwezeshwa, kwa kifupi EPRA, Bi. Zainabu Kivuyo, akielekeza na
kuandika mambo muhimu ya msingi kwa kamati ya Kijiji, wakati itakapokuwa katika
utekelezaji wa mradi.
Sehemu ya majukumu ya kamati ya Kijiji kwa
mradi huo wa barabara….
Mwezeshaji mwingine, Bwana Jabir Ally, ambaye ni
mratibu wa TASAF Wilaya ya Arusha (Arusha Vijijini), naye akiwa kazini ndani ya
semina hii, akitoa maelekezo juu ya namna ya suala zima la umuhimu wa usimamizi
wa mradi.
Mtaalamu wa masuala ya kifedha, Bwana Dixon
Andindilile, ambaye ni mhasibu (Bwana fedha) wa TASAF wilaya ya Arusha (Arusha
Vijijini), akiwa katika eneo lake la kitaaluma akiwapa mwongozo washiriki wa
semina, katika namna na jinsi masuala mazima ya kifedha (uchukuaji na utumiaji) yanavyotakiwa
kupangiliwa na kutunzwa kitaalamu kwa ajili ya ukaguzi pamoja na uhakiki. Hapa akiwaonesha
washiriki wa Semina hii hundi ya fedha jinsi ilivyo, na namna ya matumizi yake
katika mradi.
Washiriki wakiwasikiliza kwa makini wawezeshaji
wao, na huku baadhi yao
wakipewa nafasi ya kusimama na kuuliza maswali au kutaka kupewa ufafanuzi wa masuala
pamoja na mambo mbalimbali ambayo yanawatatiza ama kutoeleweka vema kwa upande wao juu ya mradi mzima, wakati Semina ilipokuwa ikiendelea.
No comments:
Post a Comment