UTAMU WA NYAMA JIKONI; NA UJUE NI WAPI HASA INAKOTOKA.


Jengo la machinjio ya mifugo yaliyopo katika Mji wa Ngaramtoni ya Juu, nje kidogo ya Jiji la Arusha katika barabara Kuu ya Arusha-Namanga-Nairobi, linavyoonekana kwa nje. Ni jengo lililojengwa pembezoni tu mwa ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Ilkiushin (Arusha Vijijini).





Hiki ni kijumba cha maliwatoni (pa kukoga na kujisaidia).




Kwa ndani.....

Mpini Wa Shoka uliwakuta vijana hawa wakifanya usafi wa nguvu baada ya kazi ya uchinjaji kukamilika kwa siku hii. Kazi ya uchinjaji wa mifugo hufanyika mapema sana asubuhi (kuanzia alfajiri.)






Nje ya maeneo ya machinjio...

Hawa jamaa kama kawaida yao kwenye machinjio kama haya huwa hawakosekani, kwa ajili ya kujitafutia na kujipatia chochote kitu.




Na hawa pia huwa hawakosekani. Wako tele kila mahali katika eneo hili.





Huduma ya maji safi inapatikana ndani ya machinjio kwa ajili usafi na shughuli nyingine zote wakati wa uchinjaji.





Hawa wamehifadhiwa ndani ya zizi hili lililopo pembeni kidogo mwa machinjio haya, wakisubiri huduma ya kuchinjwa asubuhi na mapema ya siku inayofuata.





Hawa jamaa siyo kwamba wamelala wakijipumzisha kutokana na shibe wanayoipata katika machinjio haya. La Hasha. Hapa walipo, hawa tayari ni wafu. Wamekun'gutwa (wamepigwa) risasi katika zoezi maalumu la Serikali ya halmashauri. Ni utaratibu wa halmashauri kwamba katika eneo lote la machinjio, hapatakiwi kuonekana mbwa yoyote yule akizurura ovyo ili kuepusha madhara ya aina yoyote yale ya magonjwa mbalimbali kwa watumiaji wa nyama (binadamu). Nyama kutoka katika machinjio haya ya Ngaramtoni ya Juu, husambazwa katika maeneo mengi ya Arusha na vitongoji vyake.

No comments: