WAKWETU, KULA MBOGA ZA MAJANI SIYO HADI USUBIRI UKASHAURIWE NA DAKTARI...! ANZA TU MWENYEWE ILI UITUNZE AFYA YAKO.
Mojawapo ya matuta maridadi yaliyostawishwa vema spinachi, eneo la Sekei-Jirani na ofisi za halmashauri ya wilaya ya Arusha Vijijini. Kama hizi hauzipendi, wakwetu basi tumia hata matembele au majani ya maboga...
Watunza bustani wakiwa kazini. Eneo hili la Sekei ni maarufu kwa uuzaji wa miche ya mboga za aina mbalimbali kama unavyoona hapa. Wateja wao wakubwa ni walima bustani hasa za majumbani kutoka pande mbalimbali za Mji wa Arusha. Nawe pia wakaribishwa...
No comments:
Post a Comment