MAMBO YA BARABARA NDANI YA MJI WA ARUSHA BADO YANAENDELEA... Wakati sehemu kubwa ya barabara za Mji sasa zikiwa katika mvuto na mwonekano 'mtamu' kwa watumiaji, na kuupendezesha vilivyo mji, kazi bado inasonga mbele....


Hapa ni katika barabara maarufu inayoziunganisha barabara mbili kubwa (barabara ya Sokoine inayokwenda Singida, Mwanza, Ngorongoro na hata Musoma hadi Tarime na ile ya Afrika Mashariki inayokwenda Nairobi, Kampala na kwingineko Afrika Mashariki). Kwa wenyeji wa Mji wa Arusha, barabara hii wengine wanaiita barabara ya 'kona ya Nairobi'! Na wengine wanaiita barabara ya 'Tekniko' (Technical) kwa sababu ya kupita ubavuni mwa Chuo cha Ufundi Arusha. Kwa sasa barabara hii iko katika maandalizi makubwa ya kutaka kufumuliwa, ili kuanza kusukwa upya, ambapo inatarajiwa kuwa double road. Itakuwa ikipandisha magari mawili na kushusha magari mawili

  

Matayarisho ya barabara za pembeni kabla haijaanza rasmi kubomolewa (barabara yenyewe iko upande yanakoonekana magari)





...unaiona jinsi inavyoonekana ndogo (hapo linakopita hilo gari jeupe)





Greda kazini. Siku hii ilikuwa ni hekaheka tupu za wale wenye biashara zao ndogo ndogo pembezoni mwa barabara hasa gereji bubu. Kumbe walikwishapewa taarifa kitambo tu, lakini si unaelewa tena hulka yetu sisi 'wabongo'. Yaani hadi siku ifike na kuona ni kweli kazi inaanza, ndipo na sisi tunaanza kutimka ovyo na vitu vyetu mikononi!

 

"Lakini pamoja na jitihada hizi, bado barabara nyingi za huko wanakoishi wapiga kura; Sombetini, Daraja II, Majengo, Mbauda na kwingineko kwingi barabara za mitaa ni mbovu mno" Mpini Wa Shoka


No comments: