ARUSHA TOWN. Wakati Mpini Wa Shoka ukikatiza kwenye mitaa kadhaa ya katikati ya Mji huu maarufu wa kitalii, kwenye mtaa mmoja maarufu kwa maduka ya vifaa mbalimbali na hasa vya umeme na ujenzi maeneo ya Nobo hausi (Noble House), nikawakuta hawa jamaa wakiwa katika pilikapilika chungu nzima za kikazi. Jicho likaamua liwanase kidogo...


Hili ndilo jina la duka lenyewe. Ukipata nafasi, na wewe pia fika ukajipatie huduma na vifaa kibao vya ujenzi na mambo mengine....kama vipi, unaweza tu kuwapigia.





Wakiwa kazini, (kutoka kushoto) ni msambazaji wa bidhaa kwa wateja dereva Mussa Kijiko (ki-spoon), meneja wa duka Msuya Mussa, pamoja na mkurugenzi wa P&Q General supply kijana Bonge Mahela




Kazi bila ya mipango wala kuelewana huwa haiendi na wala huwa haifanikiwi kirahisi...kwanza tujadiliane, halafu ndipo kazi zisonge mbele...






No comments: