MOSHI-KILIMANJARO. Katika harakati za taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika (Misa-Tan) kuendelea kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa wana tasnia ya habari, mwanzoni mwa mwezi wa 07/2014, Misa-Tan walikuwa ndani ya Mji wa Moshi......Niwie radhi sana kwa kuchelewa 'kukutupia' mapema uhondo huu, kutokana na msiba wa ghafla uliokuwa umenipata, kwa kufiwa na mjomba mdogo wa mke wangu-Majengo, Arusha.....
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mkoani Kilimanjaro wakiwa wamejumuishwa kwa pamoja na taasisi ya MISA-Tan ndani ukumbi wa mafunzo, katika Chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) Mjini Moshi. Yalikuwa ni mafunzo ya siku 4, katika kuiangalia fursa ya intaneti kama mlango mpya (chanzo) wa habari na mawasiliano. Mpini Wa Shoka nao pia ulikuwepo katika full makamuzi...
Washiriki, Yusuph Mazimu wa Moshi Fm (aliyeshika kidevu) na Dixon Busagaga wa Michuziblog na Freemedia wakimfuatilia kwa makini mwongozaji wa mafunzo....
Philemon Mark Sihavango-Mkurugenzi wa redio Sauti ya Injili-Moshi (kulia) na Furaha Hamadi wa Moshi FM nao pia hawakuwa nyuma...
Wakati mwingine utamu wa mafunzo uliwafanya baadhi ya washiriki wajikute katika vicheko vya raha. Kutoka kushoto ni Omari Mlekwa-gazeti la SihaLeo (Hai), Hellen Madege-Sauti ya Injili na Roman Mnzava-Boma FM (Hai)
Kutoka kulia ni Zephania Renatus-Star TV, Emmanuel Mnzava-Chuo cha uandishi wa habari (Udzungwa College), na Upendo Mosha-NewHabari
Nakajumo James-gazeti la HabariLeo, ambaye ni kiongozi wa wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro, akijaribu kupiga picha kadhaa za kumbukumbu wakati mafunzo yakiendelea huku akitazamwa kwa makini na Zephania Renatus-Star TV na Emmanuel Mnzava-Chuo cha uandishi wa habari (Udzungwa College) anayechungulia kwa pozi...
Martha Fatael (wa kwanza kushoto) wa magazeti ya Majira na Mwananchi akishirikiana jambo kwenye kompyuta na Fadhila Omari wa ITV
Wakati fulani mratibu wa mafunzo haya kutoka MISA-Tan, Andrew Mara witi (mwenye shati jeupe), naye pia alipata fursa ya kusimama mbele ya darasa na kuwasilisha masuala mawili matatu muhimu kuhusiana na mada mbalimbali ndani ya mafunzo haya. Hapa akiwa na Dixon Busagaga wakiwasilisha...
Lucy Ulomi-SihaLeo akiwa katika mazoezi kwa vitendo na Hellen Madege wa Redio Sauti ya injili...
Fadhili Athumani (aliyesimama) wa gazeti la NewHabari akielekezana jambo kwenye kompyuta na Salma Shabani Maumi wa Boma FM-Hai
Kwa hakika lilikuwa darasa tamu kwelikweli, na sote tulijifunza na kufaidika sana....
(www.dixonbusagaga.blogspot.com yeye alifanikiwa kuitoa mapema zaidi habari hii. shukurani kwake)
No comments:
Post a Comment