UBUNIFU!
Jiko kwa matumizi ya kuni. Natumaini unalifahamu vema jiko la mafiga matatu; yaweza kuwa ni mawe makubwa matatu au hata matofali, halafu katikati panaweka chungu ama sufuria tayari kwa mapishi huku kuni zikichochewa kwa mikono na kwa kupuliza kwa mdomo ili moto uwake vema, chakula kipate kuiva. Hivi karibuni Mpini Wa Shoka ukiwa maeneo ya Majengo (Arusha town) ulikutana na ubunifu wa jiko hili la kutumia kuni, mbadala wa lile jiko letu la mazoea la mafiga ya mawe au matofali! Hili unaweza hata ukalipakiza ndani ya gari ukasafiri nalo hata Johanesburg, Maputo, Nakuru, Kigali, Kagadi-Kibaale, Bujumbura na kwingineko kote, kisha mapishi yakaendelea kama kawaida! Aiseee!
Sufuria jikoni; kwa chini kuni ziwaka taratibu. Punde tu 'msosi' wa nguvu utakuwa tayari
No comments:
Post a Comment