KWA HAKIKA WAKATI WA SHEREHE AU MISIBA NDIPO HASA NAFASI NZURI YA NDUGU NA JAMAA KUKUTANA NA KUFAHAMIANA......
Mwezi wa 07/2014 (siku za mwanzo za mfungo mwezi wa Ramadhani), familia ya bibi Fatuma Mohammed "mama Hassani" ya Majengo ya juu Arusha ilikuwa katika msiba wa mtoto wa mwisho wa bibi huyu, marehemu Mussa Saidi Kivuyo, aliyezikwa Ngaramtoni ya Chini-Arusha. Katika mkusanyiko wa msiba huo nyumbani kwa bibi huyu, Majengo ya juu, ilipatikana nafasi ya watu mbalimbali wa ndani ya Arusha na nje ya Arusha na hata wa nje ya Tanzania kukutana, kuzungumza, kubadilishana mawazo na hata kufahamiana baada ya kupoteana kwa miaka kadhaa. kwenye picha hizi mbili, aliyenyoosha mkono, ni kaka wa marehemu, Daktari Hassani Saidi Kivuyo wa hospitali ya Mount Meru Arusha akisisitiza jambo alipokuwa akibadilishana mawazo na nduguze, Yussuph aliyekaa jirani naye (mwenye shati jeupe), Hamadi (aliyevaa kofia) na Husseni.
Mwenye sweta la bluu ni Mohammed Solloka, ambaye ndiye kaka mkubwa kabisa wa marehemu
Hapa kuna baadhi ya watoto wa marehemu pamoja na baadhi ya wajukuu. Waliosimama, mwenye shati la bluu ni Saidi Mussa Kivuyo (mtoto wa marehemu) na Saidi Hamadi Kivuyo (mtoto wa kaka wa marehemu). Waliokaa kutoka kushoto, mwenye kilemba cheupe ni Sadra Amour (mjukuu wa marehemu), Mansour Mussa Kivuyo (mtoto wa marehemu), Sabrina (mjukuu wa marehemu), Saidi Hamadi Kivuyo (mtoto wa kaka wa marehemu), Saidi Mustafa Kivuyo (mtoto wa kaka wa marehemu) na Salha Mussa Kivuyo (mtoto wa marehemu)
Mwenye shati la draft ni Abdillahi Mohammed "babuu" (mjomba wa marehemu) na Mohammed Solloka (kaka mkubwa wa marehemu)
No comments:
Post a Comment