HEBU JARIBU KUKADIRIA NA KUFIKIRIA... Hii ni habari iliyozagaa na kuvuma kwa muda mrefu sana. Tangu mimi nilipoanza kuisikia, ni miaka mingi imekwishapita. Ni habari juu ya jiwe kubwa (wenyewe wajuzi wanaliita RED PLANET) ambalo linakimbia kwa kasi ya hatari huko angani likielekea kuja kuigonga sayari yetu hii tunamoishi (DUNIA)! Wenyewe wajuzi wanadai kwamba ukubwa wa jiwe hili ni zaidi ya mara mbili ya ukubwa wa sayari yetu ya DUNIA. Hata mimi sielewi ni kitu gani hasa kitakachotokea, endapo kama ni kweli jiwe hili litafanikiwa kufika na kuipiga DUNIA yetu hii iliyojaa kila aina ya rundo la hekaheka, mizozo, vita, milipuko ya magonjwa ya kutisha hata yasiyokuwa na tiba, shida, matatizo, tabu; huku pakiwa na chembechembe kidoooooogo mno za raha na furaha..! Yawezekana hata JIWE hili tayari limekwishaikaribia kabisa DUNIA, na wakati wowote ule mshindo wake wa kutisha utasikika, na kila mmojawetu ajikute akitawanyika ovyo akikimbia kama jeti huku na kule kuitafuta nusura ya nafsi yake..! Sasa sijui hata tutakimbilia wapi? Eeh, Mola tuepushe na hili balaa..! Maisha tunayachezea ovyo usiku na mchana kwa madhambi tele (makubwa kwa madogo), na kumbe hatari ya kutisha iko jirani kabisa na nyoyo zetu...! Ole wetu sisi wakazi wa hii DUNIA...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment