YAANI KAMA HII NDIO INGEKUWA ILE SIKU YA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA 2014 HUKO NCHINI BRAZIL KWA 'wazee wa 7Up', BASI NAFIKIRI NYOYO ZA WAAJENTINA NA MESSI WAO ZINGEKUWA BARDIIIIIIIIIIIII; lakini wapi! HII NI MIONGONI MWA MECHI KIBAO ZA KIRAFIKI ZILIZOPIGWA MAENEO MBALIMBALI KOTE DUNIANI...
Ushindi mtamu, meku; hata kama ni mechi ya kirafiki! Wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina, Sergio Aguero (10), Zaballeta, pamoja na mshambulizi mpya wa Man 'U' ya Uingereza, Angello De Maria aliyekuwa nyota wa mchezo wakishangilia mojawapo ya mabao yao baada ya kulipiza kisasi kwa kuwafurumua vilivyo mabingwa wa dunia, Ujerumani, kwa kuwacharaza bakora 4-2.
UINGEREZA nao walikuwa uwanjani dhidi ya Norway....
Mshambuliaji, Daniel Sturidge, wa Uingereza akiwatoka walinzi wa Norway. Uingereza ilishinda 1-0 lililopachikwa na Wayne Rooney.
No comments:
Post a Comment