NI KAZI MTINDO MMOJA... NI HARAMBEE YA JASHO NA NGUVU... WANAMUME WANAPAMBANA KUHAKIKISHA KAZI INAKAMILIKA... WANAMIMINA ZEGE KATIKA UJENZI WA MSIKITI MTAA WA NDARVOI, KATA YA DARAJA II, JIJINI ARUSHA...

...Unatarajiwa kuwa ni msikiti wa ghorofa mbili.




Hapa hakuna cha Imamu wala Ustaadh, wote ni kazi tu kwa kwenda mbele...



 

Mstari kwa ajili ya kumimina zege kwenye mashimo. Kazi ilikuwa ya moto kwelikweli, kiasi cha kuwafanya baadhi yao kuziinua juu shingo zao ili kujipumzisha japo kidogo...




Zege linamiminwa kisawasawa mashimoni...



 

Hili ni mojawapo ya mashimo yaliyokuwa yakimiminiwa zege. Mashimo haya yalikuwa 6; na yote yalikamilishwa kwa ushirikiano na nguvu ya pamoja...




Huyu swahiba anaitwa Baraka. Alifanya kazi vilivyo. Lakini baada tu ya kupata 'msosi' (chakula) wa mchana, mwili ukaishiwa kabisa na nguvu; akaamua ajiweke pembeni aondoe msongamano, na kubaki akiwashuhudia wenziwe wakiliendeleza wimbi la kuchapa kazi...




Watoto nao hakuwa nyuma hata kidogo katika harambee hii ya jasho na nguvu. Nao pi walichapa kazi vilivyo... 




Baada ya mashimo yote kukamilishwa; ikawa ni kunawa, kujisafisha na pia kuvisafisha vifaa na vyombo vyote vya kazi... Ama kweli kazi ni watu...na watu ndio kama hawa...

No comments: